Page 134 - Historiayatznamaadili
P. 134
Kazi ya kufanya namba 8
Chunguza mchoro wa mfumo wa uongozi wa jadi
wa jamii za Kifalme na Kitemi, kisha eleza mfanano
na tofauti zilizopo katika mgawanyo wa madaraka
FOR ONLINE READING ONLY
katika mifumo hiyo.
Mgawanyo wa madaraka ulileta mafanikio mengi katika jamii
za kale. Mgawanyo huu ulisaidia kushirikisha watu mbalimbali
katika uongozi. Hivyo, kuwezesha shughuli za jamii na watu
kupata mahitaji yao ya msingi. Pia, mfumo wa uongozi ulitumika
kutatua migogoro katika jamii na kusimamia ulinzi na usalama
wa jamii.
Licha ya Mfalme, Rumanyika, mkoa wa Kagera ulikuwa na
watawala wengine kama Kasusura aliyetawala Biharamulo,
Rutinwa aliyetawala Kiziba na Kayoza aliyetawala Bugabo. Pia,
palikuwa na watawala wengine kama Kahigi aliyetawala Kihanja,
Nyarubamba aliyetawala Ihangiro, Lugomola aliyetawala Bukara,
na Rukamba aliyetawala Kyamtwara. Hawa walikuwa na utawala
wa kifalme katika maeneo yao.
Kazi ya kufanya namba 9
Andika sababu za kukua na kuimarika kwa utawala
wa kifalme kabla ya kuja kwa ukoloni nchini.
Utawala wa Mangi katika jamii za Wachaga
Utawala wa Mangi ni miongoni mwa tawala za Kichifu zilizokuwapo
katika mkoa wa Kilimanjaro, Kaskazini mwa Tanzania katika jamii
za Wachaga. Mfano, Mangi Sina alitawala eneo la Kibosho, Mangi
Marealle eneo la Marangu na Vunjo, Mangi Shangali eneo la
Machame na Mangi Meli eneo la Old Moshi. Uongozi wa Mangi
ulikuwa wa kurithi.
127
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 127
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 127 06/11/2024 11:30:21