Page 136 - Historiayatznamaadili
P. 136
Mangi Meli aliua baadhi ya Wajerumani na kamanda wao
aliyeitwa Von Bulow.
Wajerumani walishindwa vita
na waliondoka katika himaya
FOR ONLINE READING ONLY
yake eneo la Old Moshi kwa
muda wa mwaka mmoja na
nusu. Aidha, Wajerumani
walirudi kupigana naye
baada ya kujiimarisha kijeshi.
Hata hivyo, ilibidi Wajerumani
kutumia jeshi la Wanubi
kutoka Sudani katika jeshi
lao ili kukabiliana na Mangi Kielelezo namba 7: Mangi Meli
Meli. wa Old Moshi
Wanubi ni Waafrika na ni watu wa vita. Vita hivi vilidumu siku
mbili tu na Wajerumani walifanikiwa kuingia eneo lake. Mangi
Meli alikubali kwa shingo upande Wajerumani kuingia katika
himaya yake. Aidha, Mangi Meli aliendelea kwa siri kujijenga
kijeshi ili kuwaondoa Wajerumani katika eneo lake. Kiongozi
huyu alihamasisha jamii za Wachaga, Wameru, Wamasai, na
Wapare kuungana kijeshi ili kupinga Wajerumani kuingia katika
maeneo yao. Aidha, mpango huu haukufanikiwa kwa sababu
alisalitiwa na wenzake. Wajerumani walimkamata na kumhukumu
kifo cha kunyongwa hadharani. Hivyo, Mangi Meli alinyongwa
hadharani. Mangi Meli alikuwa kiongozi imara na shupavu, kama
siyo usaliti kutokana na ulaghai wa Wajerumani, kamwe Mangi
Meli asingeshindwa vita na kukamatwa.
Kuna Mangi wengine ambao walipinga utawala wa Wajerumani
kwa nyakati tofauti. Kielelezo namba 8, kinaonesha picha ya
baadhi ya Mangi wakiwa katika eneo la boma la Wajerumani
kujibu shitaka la kupinga utawala wa Wajerumani.
129
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 129 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 129