Page 131 - Historiayatznamaadili
P. 131
Tawala za Kifalme kabla ya ukoloni
Tawala za Kifalme zilikuwa maarufu katika maeneo ya Kaskazini
Magharibi mwa Tanzania, pembeni mwa Ziwa Victoria. Utawala
wa Kifalme ulijikita katika jamii za maeneo ya Karagwe na Buhaya.
FOR ONLINE READING ONLY
Utawala wa Kifalme ulikuwa wa kurithi na ulianzia katika utawala
wa Bachwezi na Babiito. Utawala ambao uliibuka zaidi wakati wa
biashara ya masafa marefu na wafanyabiashara toka Mashariki
ya Mbali na Kati hasa Waarabu. Utawala wa Kifalme uliisha
baada ya kufutwa kwa tawala za Kifalme na Kichifu nchini na
Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Mambo yaliyosababisha kukua kwa tawala za Kifalme nchini
Utawala wa Kifalme ulikua kutokana na shughuli za kilimo. Hii
ilitokana na uwepo wa ardhi nzuri yenye rutuba na mvua za
kutosha katika eneo la utawala wa Kifalme. Jamii za Kifalme
zilijishughulisha sana na shughuli za kilimo cha mazao ya chakula,
na hata kuzalisha ziada ambayo ilitumika kwa ajili ya biashara na
jamii zilizowazunguka.
Ugunduzi wa chuma wakati wa utawala wa “Ndagara” katika
maeneo ya Karagwe kulichangia zaidi kukua kwa himaya za
Kifalme maeneo ya Buhaya na Karagwe kabla ya ukoloni.
Ugunduzi huo ulisababisha kukua kwa viwanda vya ufuaji chuma
na kutengeneza zana imara za kilimo kama vile majembe,
mashoka, mapanga na mundu. Zana hizi zilichangia kuongeza
maendeleo katika shughuli za kilimo, kwani wakulima waliweza
kulima maeneo makubwa zaidi na kupata mazao ya chakula na
ziada kwa ajili ya biashara.
Vilevile, ugunduzi wa chuma ulisaidia jamii hizi kutengeneza
zana za vita na uwindaji kama vile mishale, mikuki na mapanga.
Zana hizi zilitumika kwa ajili ya ulinzi na upanuzi wa himaya za
Kifalme. Pia, zilitumika katika biashara ili kupata bidhaa ambazo
124
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 124 06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 124