Page 128 - Historiayatznamaadili
P. 128
bila kushindwa kutokana na
mbinu za kivita alizokuwa
nazo. Alitumia nyuki na silaha
za jadi kushinda vita dhidi ya
FOR ONLINE READING ONLY
wavamizi katika eneo lake.
Mtemi huyu alitumia nguvu
za asili kuwakusanya nyuki
na kuwatuma kuyazingira
majeshi ya Wajerumani
waliomwendea kwa lengo la
kumuua. Kielelezo namba
3, kinaonesha Mtemi Litti Kielelezo namba 3: Mtemi Litti
Kidanka. Kidanka
Nyuki walitumwa kila majeshi ya Wajerumani yalipomkaribia
na kuikaribia himaya yake. Nyuki hao waliwauma majeshi
hayo kulingana na maagizo ya mtemi huyu. Hivyo, Wajerumani
walikimbia ili kuokoa maisha yao. Mapambano dhidi ya
Wajerumani yalichukua zaidi ya miaka mitatu. Mtemi Litti
alipambana na Wajerumani mara mbili na kuwashinda. Safari
ya tatu Mtemi Litti hakuweza kufanikiwa kuwashinda kutokana
na usaliti uliofanywa na baadhi ya maadui zake. Hii ilisababisha
Wajerumani kufanikiwa kumuua na kukata kichwa chake na
kukipeleka Ujerumani na hakijarejeshwa nchini hadi leo.
Kazi ya kufanya namba 5
Jadili madhara ya usaliti katika ulinzi na usalama wa
jamii zetu hapo kale na sasa.
Mutwa (mtemi) Mkwawa
Mutwa Mkwawa Mukwavinyika Mwamuyinga alikuwa mtawala
wa jamii ya Wahehe. Milki ya utawala wa Mutwa Mkwawa ilikuwa
katika Mkoa wa Iringa, eneo la Kalenga. Kiongozi huyu alijulikana
121
06/11/2024 11:30:21
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 121
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 121 06/11/2024 11:30:21