Page 123 - Historiayatznamaadili
P. 123
Kwa mfano walijulikana kwa majina ya Abakama, Watwa,
Mangi, Watemi na kadhalika. Viongozi hawa waliheshimika sana
katika himaya zao. Hii ni kwa sababu ya umaarufu na nguvu
zilizotokana na uhodari wa vita, umiliki wa maeneo makubwa na
yenye rasilimali za jamii, nguvu za asili na utawala. Hapakuwapo
FOR ONLINE READING ONLY
na mtu aliyeweza kuwapinga watawala hawa kutokana na nguvu
na mamlaka walizokuwa nazo.
Viongozi hawa walipatikana kupitia uchaguzi, urithi, ushupavu
wa kivita na umaarufu wa mtu katika kutenda kazi au uganga.
Aidha, kiongozi katika jamii alipaswa awe ni mpenda watu, awe
na tabia njema na anapenda kufanya kazi kwa bidii. Pia, ilikuwa
mwiko kwa jamii kutawaliwa na mtu mvivu, asiyependa watu au
mwenye tabia mbaya.
Kazi ya kufanya namba 2
Jadili mambo yanayofanana na kutofautiana katika
uchaguzi wa viongozi wa sasa na wa kabla ya
ukoloni.
Utawala wa viongozi wa jadi katika jamii
Kazi ya kufanya namba 3
Soma matini mbalimbali ikiwemo maktaba mtandao
kuhusu mamlaka za jadi katika jamii za Kitanzania
kabla ya ukoloni.
Utawala wa Watemi
Mfumo wa Kitemi ulianza katika jamii za Wanyamwezi. Baadaye
ulisambaa katika maeneo ya Usukuma, Usangu, Uhehe, Ukimbu,
Ugogo, Ubena na maeneo mengine ya nchi. Uongozi huu ulitumia
jina “Mtemi” kutokana na namna mamlaka zilivyoundwa. Neno
mtemi linatokana na neno “kutema” lenye maana ya “kukata” kwa
ajili ya kuongeza ardhi mpya. Jamii zilizokuwa na mamlaka za
116
06/11/2024 11:30:20
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 116
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 116 06/11/2024 11:30:20