Page 125 - Historiayatznamaadili
P. 125
Baadhi ya viongozi wa jadi waliokuwa na mfumo wa Watemi ni
Mtemi Mirambo wa Unyamwezi, Isike wa Unyanyembe, Mkwawa
wa Uhehe na Mazengo wa Ugogo. Hawa ni baadhi tu ya viongozi
wa jadi waliotumia mfumo wa utawala wa Watemi.
FOR ONLINE READING ONLY
Mtemi Mirambo
Mtemi Mirambo alikuwa kiongozi wa jamii ya Wanyamwezi (1840
– 1880). Utawala wa Mtemi Mirambo ulikuwa wa kurithi kutoka kwa
baba yake Mtemi Kasanda wa Uyowa. Uyowa ni eneo la utawala
wa baba yake. Kielelezo namba 1 kinaonesha picha ya Mtemi
Mirambo.
Tangu awali himaya hii ilikua kutokana na uwezo mkubwa wa
kijeshi waliokuwa nao. Aidha, utawala huu ulikua zaidi kutokana
na uvamizi wa maeneo yaliyowazunguka ili kupanua himaya.
Mfano, Mtemi Mirambo
aliendeleza utawala wa
himaya hii baada ya kifo
cha baba yake kwa kuvamia
maeneo yaliyowazunguka
kama vile Ulyankulu na
kuunganisha na Uyowa,
hivyo kuanzisha utawala wa
Urambo.
Kama zilivyo tawala zingine
za Kitemi, utawala huu
uliimarika zaidi kutokana
na biashara za masafa
marefu na zile zilizofanyika
katika Pwani ya Bahari
ya Hindi. Jamii hii ya
Wanyamwezi ilikuwa moja
ya jamii maarufu sana
katika biashara.
Kielelezo namba 1: Mtemi
Mirambo
118
06/11/2024 11:30:20
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 118
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 118 06/11/2024 11:30:20