Page 121 - Historiayatznamaadili
P. 121
Zoezi la jumla
1. Je, ni kwa nini mfumo wa ujima uliweza kujenga misingi
ya haki na usawa katika jamii?
2. Ni mambo yapi yalisababisha kuvunjika kwa misingi ya
haki na usawa wakati wa mfumo wa ukabaila katika jamii
FOR ONLINE READING ONLY
kabla ya ukoloni?
3. Fafanua sababu za kuzuka uhusiano wa kibiashara baina
ya jamii za Watanzania kabla ya ukoloni.
4. Taja mabadiliko ya kiuchumi yaliyosababishwa na kukua
kwa biashara ya masafa marefu kabla ya ukoloni.
5. Ni mabadiliko yapi ya kijamii yaliyosababishwa na kukua
kwa biashara ya masafa marefu kabla ya ukoloni?
6. Je, ni kwa namna gani biashara za masafa marefu
zilisababisha kukua kwa shughuli za kiuchumi kabla ya
ukoloni?
7. Bainisha sababu ya kuimarika kwa tawala za kijamii wakati
wa biashara ya masafa marefu na wageni toka Mashariki
ya Kati.
Msamiati
Biashara ya biashara iliyokuwa ikifanywa na jamii za
masafa marefu kale baina ya Pwani na maeneo ya ndani
ya Tanzania
Dola mamlaka katika eneo fulani, mathalani
katika nchi
Karne muda wa miaka mia moja
Mwinyi kiongozi au mtu aliyekuwa na heshima na
dhamana ya uongozi na utawala katika
maeneo ya ukanda wa Pwani
Mtwana mtu aliyekuwa chini ya Mwinyi na
aliwajibika kumtumikia
Ushuru ni kodi inayotozwa kwa bidhaa au shughuli
maalumu
114
06/11/2024 11:30:19
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 114
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 114 06/11/2024 11:30:19