Page 117 - Historiayatznamaadili
P. 117
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 3: Njia za biashara ya masafa marefu
Awali, uhusiano wa kibiashara kati ya wageni kutoka Mashariki
ya Mbali na Kati na wafanyabiashara wakubwa wa masafa marefu
ulihusisha kubadilishana dhahabu na miti ya mikoko iliyopatikana
maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi. Bidhaa nyingine zilikuwa
vipusa, ngozi za chui na magamba ya kobe zilizopatikana maeneo
ya ndani ya nchi. Dhahabu ilitoka Zimbabwe kupitia bandari ya
Sofala iliyopo Msumbiji. Biashara hii ndiyo iliyosababisha kukua
kwa miji ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kama vile
Kilwa Kisiwani.
110
06/11/2024 11:30:18
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 110
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 110 06/11/2024 11:30:18