Page 114 - Historiayatznamaadili
P. 114
Jamii za wachongaji zilibadilishana bidhaa kutoka kwa wahunzi
na wakulima kutoka kwa wafugaji. Wahunzi vivyo hivyo,
walibadilishana bidhaa zao kwa nafaka kutoka kwa wakulima,
wachongaji na wafugaji. Wakulima walibadilishana mazao na
FOR ONLINE READING ONLY
wahunzi ili kupata zana za kilimo. Pia, wakulima walibadilisha
mazao yao na jamii za wawindaji ili kupata mawindo kutoka kwa
wawindaji. Pia, wawindaji walibadilishana mawindo na wahunzi
ili kupata zana za chuma kama vile mikuki, mishale na visu.
Uhitaji katika jamii ndio uliosababisha ushirikiano na uhusiano
katika jamii kwa lengo la kupata bidhaa zilizokosekana katika
jamii zao. Biashara hizi awali zilifanyika kwa lengo la kujikimu
na siyo kupata faida kama ilivyo sasa.
Aidha, kadiri muda ulivyozidi kwenda, baadhi ya vitu vilianza
kutumika kama kipimo katika ubadilishanaji. Mfano wa bidhaa
zilizochukua hadhi ya vipimo ni zana za chuma na chumvi.
Bidhaa hizi zilitumika kama vile itumikavyo fedha sasa. Hii ni
kwa sababu kila mtu alihitaji bidhaa hizi. Mfano, idadi fulani
ya zana za chuma (majembe, mashoka, mapanga, mikuki)
ilitumika kununulia mifugo na nafaka mbalimbali. Hivyo, watu
walilinganisha thamani ya bidhaa na kubadilishana. Jamii
ziliweza kujitosheleza katika mahitaji ya chakula na uzalishaji
mali kama ilivyo sasa. Kimsingi, ushirikiano na uhusiano huu kwa
kiasi kikubwa ulikuza shughuli za biashara kabla ya ukoloni. Hali
hii ilipanua wigo kutoka biashara kati ya jamii za jirani mpaka
jamii za mbali. Jamii zilianza kusafiri hadi jamii zingine kufanya
biashara, hivyo kukua kwa biashara za masafa marefu katika
jamii.
Biashara za masafa marefu
Ushirikiano na uhusiano huu ulitambulika kama biashara za
masafa marefu kwa sababu, jamii moja ilisafiri umbali mrefu ili
kubadilishana bidhaa zilizokosekana katika jamii zao. Biashara
107
06/11/2024 11:30:18
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 107 06/11/2024 11:30:18
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 107