Page 111 - Historiayatznamaadili
P. 111
Licha ya shughuli za kuzalisha mali, jamii zilishirikiana katika
masuala ya jamii kama vile sherehe, majanga na michezo. Watu
walishiriki kwa kukaa pamoja, kula, kuimba na kucheza. Ushiriki
huu ulisaidia kujenga uhusiano mwema katika jamii za kale.
FOR ONLINE READING ONLY
Zoezi namba 2
1. Eleza mambo uliyojifunza kutokana na ushirikiano na
uhusiano wa jamii wakati wa mfumo wa ujima.
2. Eleza tofauti ya ushirikiano na uhusiano uliokuwapo
katika jamii enzi za ujima na sasa.
Ushirikiano na uhusiano wa kijamii katika misingi ya ukabaila
Kadiri maendeleo ya jamii yalivyokua ndivyo ushirikiano na
uhusiano katika jamii ulivyobadilika. Pamoja na jamii za kale
kuendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali, taratibu
misingi ya ushirikiano na uhusiano ilianza kubadilika. Mfano,
ugunduzi wa zana za chuma, ulileta mabadiliko katika mfumo
wa maisha ya binadamu. Ugunduzi wa chuma uliwezesha watu
kulima eneo kubwa zaidi na kuwa na ziada. Hivyo, baadhi ya
watu walianza kumiliki maeneo makubwa zaidi ya watu wengine.
Huu ukawa ndio mwanzo wa matabaka katika jamii na kuanza
kuvunjika kwa misingi ya ushirikiano na uhusiano uliyojengwa
katika ujima. Matabaka ya watawala na watawaliwa yalianza
kukua. Tabaka la watawala lilikuwa na mali, kwani walimiliki
ardhi kubwa. Tabaka tawaliwa halikuwa na umiliki wa ardhi.
Tabaka la waliojilimbikizia ardhi lilianza kunyonya watu wengine
kwa kuwapa maeneo ya mashamba na mifugo, kisha kudai fidia
kama ushuru. Huu ukawa mwanzo wa mfumo wa ushirikiano na
uhusiano wenye msingi ya kiunyonyaji katika jamii uliojulikana
kama “ukabaila”.
104
06/11/2024 11:30:17
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 104
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 104 06/11/2024 11:30:17