Page 110 - Historiayatznamaadili
P. 110
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1: Zana za mawe zilizowekwa mpini
Watu wote walifanya kazi pamoja katika kipindi cha ujima. Mfano
katika shughuli za uwindaji, waliwinda pamoja na mawindo
yaliyopatikana waligawana kwa usawa. Aina hii ya ushirikiano
na uhusiano iliondoa mianya ya unyonyaji, ubaguzi na dhuluma
kutokana na kuwapo kwa usawa katika umiliki na ugawaji wa
rasilimali. Pia, kutafuta maslahi kwa pamoja kuliongeza uhusiano
katika jamii za kale. Umiliki wa rasilimali katika jamii kama mifugo
na ardhi ulikuwa wa pamoja na siyo wa binafsi. Hii iliondoa
matabaka, ya wale wenye nacho kwa wingi na wasiokuwa nacho.
Watu wote walikuwa sawa. Mgawanyo wa kazi wakati wa ujima
ulizingatia jinsi na rika. Hii ilisaidia kuweka usawa katika kazi
kulingana na uwezo, uzoefu, umri na majukumu katika jinsi. Kila
mtu alifanya kazi kwa kujituma na kwa bidii. Mfumo wa ujima
ulikuwapo zaidi katika hatua za awali za maendeleo ya jamii.
Mfumo wa ujima ulisaidia kukuza ushirikiano na uhusiano wenye
misingi ya usawa katika jamii za kale.
103
06/11/2024 11:30:17
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 103
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 103 06/11/2024 11:30:17