Page 113 - Historiayatznamaadili
P. 113
Zoezi namba 3
1. Eleza misingi ya ushirikiano na uhusiano wakati wa
ukabaila.
2. Je, ni mambo yapi ya kujifunza kutokana na ushirikiano
FOR ONLINE READING ONLY
na uhusiano katika ukabaila?
3. Eleza mambo uliyojifunza kuhusu ushirikiano na uhusiano
wa kijamii kabla ya ukoloni.
Ushirikiano na uhusiano katika uchumi
Ushirikiano na uhusiano katika uchumi ulijengwa zaidi katika
misingi ya biashara kati ya jamii moja na nyingine. Ushirikiano
na uhusiano huu ulianza taratibu ambapo jamii moja na nyingine
zilibadilishana bidhaa walizozalisha. Ushirikiano na uhusiano huu
ulisababishwa na uwapo wa shughuli tofauti za uchumi, kama
vile kilimo, ufugaji, uvuvi, uhunzi, ususi, uchongaji na kadhalika.
Hii ilisababisha uhitaji kati ya jamii na jamii. Hivyo, jamii zilianza
kushirikiana na kuhusiana kibiashara kwa kubadilishana bidhaa
kwa bidhaa kati ya kaya na kaya, jamii na jamii na hatimaye na
jamii za mbali. Kielelezo namba 2, kinaonesha watu wakifanya
biashara za kubadilishana.
Kielelezo namba 2: Watu wakibadilishana bidhaa kwa bidhaa
106
06/11/2024 11:30:17
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 106
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 106 06/11/2024 11:30:17