Page 116 - Historiayatznamaadili
P. 116
Wafipa. Wafipa na Wakinga walikuwa maarufu kwa uhunzi.
Hivyo, walibadilishana bidhaa za chuma na Wakisi ili kupata
bidhaa za ufinyanzi na samaki kutoka ziwa Nyasa. Ubora wa
vyungu vya Wakisi uliwawezesha kufanya biashara mpaka
FOR ONLINE READING ONLY
Malawi. Wanyakyusa walibadilishana mazao ya chakula ili
kupata bidhaa zingine.
Sehemu za Magharibi na Kaskazini Magharibi mwa Tanzania,
jamii za Wanyamwezi, Wahaya na Wasukuma zilikuwa maarufu
katika biashara hii. Ushirikiano na uhusiano wa kibiashara
ulikuwapo baina ya jamii za Wasukuma, Wanyamwezi na
Wahaya. Biashara hii baadaye ilikwenda hadi maeneo ya nchi
za Burundi, Rwanda, Bunyoro, Buganda na Kongo (Katanga) ya
leo. Bidhaa katika biashara hii zilikuwa chumvi kutoka Uvinza,
zana za chuma kutoka Karagwe na Bunyoro, shaba kutoka
Katanga, kahawa kutoka Buhaya na nguo za miwale kutoka
Kongo. Chumvi ya Uvinza ilikuwa maarufu sana kama bidhaa
katika biashara hii. Biashara za masafa marefu zilisababisha
kukua kwa shughuli za uchumi zilizochochewa na uhitaji wa
bidhaa katika biashara. Kielelezo namba 3, kinaonesha njia za
biashara za masafa marefu.
Biashara za Masafa Marefu Pwani ya Bahari ya Hindi
Ushirikiano na uhusiano wa biashara za masafa marefu ulikuwa
zaidi hadi kuhusisha jamii za Pwani ya Bahari ya Hindi. Ujio
wa wageni kutoka Mashariki ya Mbali na Kati katika maeneo
ya Pwani ya Bahari ya Hindi ulisababisha wafanyabiashara
wakubwa, hasa waliomiliki biashara za masafa marefu kuanza
kufanya biashara na wageni hao. Hii ilisababisha kukua zaidi
kwa ushirikiano na uhusiano wa kibiashara nchini.
109
06/11/2024 11:30:18
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 109
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 109 06/11/2024 11:30:18