Page 138 - Historiayatznamaadili
P. 138
Mwinyi Mkuu alikuwa mtu wa kuheshimika sana. Mwinyi alipopita
mahali, watu wote walilazimika kupiga magoti. Pia, mtu yeyote
aliyekuwapo juu ya paa la nyumba au juu ya mti kwa muda
huo alilazimika kushuka mpaka Mwinyi alipopita. Wavuvi wote
FOR ONLINE READING ONLY
waliporudi kuvua samaki walilazimika kupeleka samaki wazuri na
wakubwa kwa Mwinyi Mkuu. Wafugaji nao walilazimika kupeleka
nyama ya nundu kila wachinjapo ng’ombe kwa Mwinyi. Hii ni
kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kula nyama ya
nundu zaidi ya Mwinyi. Jamii hizi ziliamini kwamba nyama ya
nundu ina mafuta mengi hivyo, ilipaswa kuliwa na mtawala.
Utawala huu msingi wake mkubwa ulikuwa kumiliki ardhi.
Tabaka la mamwinyi pekee ndilo lililomiliki ardhi. Ardhi ya
mamwinyi ililimwa mazao ya chakula na biashara kama vile
mpunga na minazi. Mamwinyi waliwatumia watumwa na
watwana katika kuhudumia mashamba yao. Mfano, maeneo
ya Zanzibar yaliyokuwa chini ya himaya ya Mwinyi Mkuu ni
Mfenesini, Ndagaa, Kikungwi, Mchangani, Chwaka, Marumbi,
Uroa, Pongwe na Unguja Ukuu. Utawala wa Umwinyi ulisaidiwa
na Wajumbe na Masheha. Viongozi hao walipokea maagizo
kutoka kwa Mwinyi Mkuu na kuwapelekea wananchi kwa ajili
ya utekelezaji.
Kazi ya kufanya namba 10
Soma matini mbalimbali kuhusu tawala za kifalme
na kimwinyi kabla ya ukoloni, kisha andika tofauti
za tawala hizo.
Mamlaka za kirika
Jamii zilizokuwa na mfumo wa kiutawala wa rika ni jamii za
wafugaji, mfano Wamasai. Mfumo wa utawala wa kirika,
ulijulikana hivyo kwa kuwa uligawa mamlaka au madaraka
kulingana na umri au rika. Mfano, jamii ya Wamasai ilikuwa na
131
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 131 06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 131