Page 143 - Historiayatznamaadili
P. 143
Zoezi la jumla
1. Eleza sababu kuu tatu (3) za kukua kwa mamlaka za
viongozi wa jadi kabla ya kuja kwa ukoloni nchini.
FOR ONLINE READING ONLY
2. Andika neno NDIYO mbele ya sentensi ambayo ni kweli
na neno HAPANA mbele ya sentensi ambayo si kweli.
(i) Mojawapo ya jukumu la viongozi wa jadi ni
kusimamia masuala ya mila na desturi za jamii
zao ____________
(ii) Biashara za masafa marefu zilisaidia kukua kwa
mamlaka za viongozi wa jadi kabla ya ukoloni
____________
(iii) Viongozi wa jadi waliruhusu kirahisi wageni kuingia
katika himaya zao __________________
(iv) Mamlaka za kirika zilikuwa na mchango mkubwa
katika kuleta maendeleo ya jamii zao_____________
(v) Ugunduzi wa chuma ulichangia kukua na kuimarika
kwa mamlaka za jadi nchini______________
3. Je, ni mafanikio gani yaliyosababishwa na mamlaka za
jadi nchini kabla ya ukoloni?
4. Eleza ni jinsi gani ugunduzi wa chuma ulichangia kukua
na kuimarika kwa mamlaka za jadi nchini.
5. Je, tunawezaje kuendeleza mbinu za uongozi zilizotumiwa
na mamlaka za jadi katika kuleta maendeleo nchini kwa
sasa?
Msamiati
Jadi asili, kale au chanzo cha jambo fulani
Himaya eneo la utawala wa kiongozi mmoja, mara nyingi
huwa na mipaka
Mamlaka nguvu au uwezo aliopewa kiongozi katika eneo
fulani ya kiutawala na maamuzi
136
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 136
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 136 06/11/2024 11:30:22