Page 147 - Historiayatznamaadili
P. 147
(d) Kulinda maadili ya jamii zao dhidi ya uharibifu kutoka
kwa wageni. Mamlaka za jadi zililinda jamii zao dhidi ya
mwingiliano wa maadili ya kigeni. Hivyo, zilipiga marufuku
mawazo, itikadi au mifumo ya maisha, mila na desturi
zilizokuwa tofauti na za jamii zao. Mfano, mamlaka za
FOR ONLINE READING ONLY
Wangoni zilipinga mfumo wa kilimo ulioletwa na Wajerumani
baada ya kugundua kuwa ulikiuka maadili ya mababu zao.
Vita ya Majimaji chini ya Kinjekitile Ngwale, inaweza ikawa
na sababu nyingi, lakini sababu za msingi zilitokana na
Wajerumani kuvuruga maadili ya jamii za watu wa Kusini
mwa Tanzania. Aidha, ulinzi wa maadili ulienda sambamba
na kurithisha maadili ya jamii zao kutoka kizazi kimoja hadi
kingine.
Zoezi namba 1
1. Bainisha mchango wa mamlaka za jadi katika kukuza
na kutunza maadili nchini.
2. Eleza mambo ya kuendeleza katika kukuza na kutunza
maadili nchini kwa sasa.
Mbinu zilizotumika katika ukuzaji na utunzaji wa maadili
Mamlaka za jadi zilitumia mbinu mbalimbali katika kukuza na
kutunza maadili ya jamii kama vile:
(a) Ibada za kijadi. Ibada zilizoambatana na matambiko
zilifanyika ili kuomba nguvu za miungu, malaika na mizimu ya
jamii kusimamia maadili. Jamii iliamini iwapo mtu angekiuka
maadili na ibada za matambiko zingefanyika, angeweza
kupata laana na kukumbwa na majanga. Mfano, mhusika
kuwa mwehu, kutokuzaa, kukosa mafanikio katika maisha,
kupata ugonjwa usiotibika na kadhalika. Hii ilisababisha
jamii kuzitii mamlaka za jadi katika usimamizi wa maadili
ya jamii kwani zilisimamia miungu ya jamii.
140
06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 140 06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 140