Page 142 - Historiayatznamaadili
P. 142
Mafanikio yaliyopatikana kutokana na mfumo wa uongozi
wa jadi
Viongozi wa jadi walisababisha maendeleo makubwa katika
tawala zao. Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio ya tawala za jadi
FOR ONLINE READING ONLY
kabla ya ukoloni:
(a) Kupanuka na kuimarika kwa mamlaka za jadi katika jamii
zao kama vile za Wafalme, Watemi, Machifu, Mangi na
kadhalika. Mamlaka hizo zilisaidia wakati wa harakati za
kudai uhuru;
(b) Kuwaunganisha watu, hivyo, kuwa na umoja, heshima
na ushirikiano kati ya wanajamii;
(c) Kupambana na wavamizi wa ukoloni katika maeneo
yao, hivyo, kujenga chachu ya kupinga ukoloni nchini;
(d) Kutatua na kuondoa migogoro ndani ya jamii na kuleta
amani, utulivu na ustawi wa jamii;
(e) Kujenga misingi ya kupenda kazi katika jamii;
(f) Kuimarisha na kukuza shughuli za uchumi katika jamii,
hivyo watu kuzalisha kwa matumizi binafsi na ziada;
(g) Kupanuka kwa ujenzi wa makazi;
(h) Kuondoa migogoro ya ardhi kwa kuweka utaratibu mzuri
wa matumizi ya ardhi;
(i) Kulinda utamaduni wa jamii; na
(j) Kuimarisha mgawanyo na usimamizi mzuri wa kazi.
Kazi ya kufanya namba 13
Soma matini kuhusu utawala wa jadi, kisha andika
taarifa fupi kuhusu viongozi watano (5) wa jadi
ambao hawakutajwa katika sura hii.
135
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 135 06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 135