Page 145 - Historiayatznamaadili
P. 145
inafuata maadili ya jamii husika. Hii ilisaidia jamii kufuata maadili
yaliyokubalika na jamii nzima. Aidha, mifumo hii ilishirikiana na
kutegemeana katika kukuza na kutunza maadili.
Kazi ya kufanya namba 2
FOR ONLINE READING ONLY
Jadili namna mamlaka za jadi zinavyosimamia
ukuzaji na utunzaji wa maadili katika ukoo.
Mamlaka za jadi
Jamii zilikuwa na koo mbalimbali, ambazo zilikuwa chini ya
mamlaka za jadi. Mamlaka za jadi zilikuwa na viongozi wakuu,
ambao walijulikana kama Machifu, Watemi, Mutwa Mangi au
Wafalme (Omukama). Mfano wa viongozi hawa wa jadi nchini
ni Mtemi Mirambo na Isike wa kabila la Wanyamwezi, Mutwa
Mkwawa wa kabila la Wahehe, Omukama Rumanyika wa kabila
la Wahaya, Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho,
Mangi Mareale wa Marangu na kadhalika. Mamlaka za jadi
zilikuwa na majukumu ya kuongoza shughuli zote za kisiasa,
kiuchumi na kijamii pamoja na maadili katika jamii zao. Pia,
zilikuwa na mamlaka juu ya rasilimali za jamii kama vile ardhi na
mifugo. Vilevile, walimiliki miungu ya jamii. Kimsingi, mamlaka
za jadi zilikuwa na nguvu. Hivyo, kuogopwa na watu wote katika
jamii.
Aidha, mamlaka hizo zilishirikiana na baraza lililoshirikisha
viongozi wa koo zote katika kukuza na kutunza maadili ya jamii
zao. Pia, zilishirikisha watu wenye maarifa mbalimbali katika
kabila, kama vile waganga, watu wenye stadi na maarifa ya
kiufundi, viongozi wa dini za jadi na watabiri katika ukuzaji na
utunzaji wa maadili. Watabiri walitumika kutoa taarifa za mambo
yajayo. Watu hawa walimsaidia kiongozi kwa karibu katika
kutimiza majukumu yake.
138
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 138
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 138 06/11/2024 11:30:22