Page 149 - Historiayatznamaadili
P. 149
jamii nzima kufuata mila na desturi za jamii. Elimu ilisaidia
kurithisha maadili ya jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Vijana walitegemewa na ukoo, kuendeleza mila, kanuni,
desturi na tunu walizorithishwa.
FOR ONLINE READING ONLY
(e) Sanaa, ubunifu na michezo. Jamii za jadi hazikuwa na
mifumo ya kuandika na kusoma ili kutunza kumbukumbu
za maadishi kama ilivyo sasa. Hivyo, sanaa, ubunifu na
michezo vilitumika katika kukuza na kusimamia maadili.
Mifumo hii ilisimamiwa na mamlaka za jadi ili kuhakikisha
ushiriki wa jamii na utoaji wa taarifa zinazoendana na
maadili ya jamii husika. Pia, nyimbo zilitumika kuwasifu
watu wenye maadili au kuwakanya wasio na maadili.
Kazi ya kufanya namba 4
Jadili umuhimu wa kuendeleza mbinu zilizotumiwa
na mamlaka za jadi katika kukuza na kutunza maadili
kwa sasa.
Sanaa, ubunifu na michezo katika kukuza na kutunza maadili
Mfano wa mifumo ya sanaa, ubunifu na michezo iliyotumika ni
kama ifuatavyo:
(i) Uchoraji. Jamii zilichora michoro mbalimbali ili kuonesha
shughuli za jamii na maadili yake. Michoro hii ilitumika
kama njia ya kutunza kumbukumbu kutoka kizazi kimoja
hadi kingine. Mfano wa michoro hii ni ile iliyopo mapango
ya Kondoa Irangi, Igeleke, Iringa, na Kombangulu, Kilolo.
Michoro hii ilitunzwa na kusimamiwa na mamlaka za jadi.
Kielelezo namba 1, kinaonesha michoro inayoelezea
shughuli za uchumi na maadili ya jamii.
142
06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 142 06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 142