Page 151 - Historiayatznamaadili
P. 151
(iii) Uchongaji. Uchongaji wa vitu kama vile vinyago
ulifanyika ili kuonesha maisha mbalimbali ya jamii. Kuna
vinyago vilivyochongwa ili kusisitiza umoja, ushirikiano
au upole. Vingine vilionesha heshima, utii kwa wakubwa,
FOR ONLINE READING ONLY
kusaidia wasiojiweza na kupendana. Mbinu hii ilisaidia
kutoa taarifa na kutunza kumbukumbu za jamii kwani
vinyago vilidumu hadi vizazi vilivyofuata, hasa vile
vilivyochongwa kwenye mti mgumu au jiwe. Kielelezo
namba 2, kinaonesha vinyago vyenye kutoa ujumbe
wa maadili ya jamii.
Kielelezo namba 2: Vinyago vyenye ujumbe wa mila na desturi za jamii
Zoezi namba 3
1. Orodhesha vitu unavyoviona katika picha namba 1, 2
na 3.
2. Eleza tafsiri ya vitu ulivyoorodhesha katika swali la 1.
(iv) Simulizi. Simulizi mbalimbali kama vile, riwaya (hadithi),
tamthiliya, michezo ya kuigiza, ushairi, na ngano zenye
maudhui mahususi ya maadili kwa jamii zilitumika
kukuza na kutunza maadili ya jamii husika. Simulizi
hizi ziliwafundisha watu maadili ya jamii. Kadiri simulizi
zilivyosimuliwa, zilirithishwa kizazi kimoja hadi kingine.
144
06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 144 06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 144