Page 154 - Historiayatznamaadili
P. 154
adhabu kwa usawa kulingana na kosa husika. Mamlaka
za jadi zilikuza na kusimamia maadili ya jamii kwa maslahi
ya jamii zao. Misingi hii ilisaidia kuwapo kwa uaminifu na
heshima pale viongozi wa jamii waliposisitiza na kusimamia
FOR ONLINE READING ONLY
ukuzaji na utunzaji wa maadili ya jamii.
(c) Umoja. Viongozi wa jadi walisimamia maadili kwa kushirikina
na mamlaka zingine kuanzia ngazi ya familia na ukoo. Hii
ilirahisisha ukuzaji na utunzaji wa maadili katika jamii nzima.
Baadhi ya makosa yalipotokea, familia au ukoo uliwajibika
kwa kutokukuza na kutunza maadili katika ngazi zao. Hii
ilisababisha mamlaka za familia na koo kuwa mstari wa
mbele katika kusimamia ukuzaji na utunzaji wa maadili
katika jamii.
Kazi ya kufanya namba 8
Jadili mambo uliyojifunza kuhusu misingi ya ukuzaji
na utunzaji wa maadili iliyotumiwa na mamlaka za
jadi na jinsi ya kuiendeleza kwa sasa.
Wajibu wa mtoto katika kukuza na kutunza maadili
Kazi ya kufanya namba 9
Fikiri na andika wajibu wako katika kukuza na
kutunza maadili ya jamii kwa sasa.
Ukuzaji na utunzaji wa maadili katika jamii ni jukumu la kila mtu.
Hivyo, kama mtoto unao wajibu wa kufanya mambo yafuatayo
katika kukuza na kutunza maadili ya jamii:
(a) Kujifunza. Mtoto anaweza kujifunza maadili akiwa
nyumbani, shuleni na katika jamii inayomzunguka. Mtoto
anaweza kujifunza maadili ya jamii kwa kusikiliza, kusoma
ama kuiga vitendo vya kimaadili kutoka kwa wazazi, walezi,
147
06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 147 06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 147