Page 156 - Historiayatznamaadili
P. 156
Mtoto anapaswa kuwa sehemu ya kukuza na kutunza maadili
ya jamii ili kuwezesha mwendelezo wa maadili ya jamii kutoka
kizazi kimoja hadi kingine.
Zoezi namba 5
FOR ONLINE READING ONLY
1. Taja vitendo vinavyoashiria ukiukwaji wa maadili katika
mazingira yako.
2. Je, ni mambo yapi ya kuzingatia wakati wa utoaji wa
taarifa za ukiukwaji wa maadili?
3. Taja mamlaka za kisheria zinazosimamia ukiukwaji wa
maadili katika jamii.
4. Je, kuna umuhimu gani wa kutunza siri wakati wa kuripoti
matukio ya ukiukwaji wa maadili?
Zoezi la jumla
1. Eleza mbinu ambazo mamlaka za jadi zilitumia katika
kukuza na kutunza maadili ya jamii zao.
2. Je, ni kwa namna gani viongozi wa sasa wanaweza
kukuza na kutunza maadili ya jamii?
3. Je mtoto anawezaje kuwa sehemu ya kukuza na kutunza
maadili ya jamii yake?
4. Eleza umuhimu wa jamii nzima kushiriki katika ukuzaji na
utunzaji wa maadili ya jamii.
5. Eleza namna ambavyo muziki wa kizazi kipya umechangia
katika kukuza maadili ya jamii kwa sasa.
6. Eleza namna ambavyo muziki wa kizazi kipya umechangia
katika kuharibu maadili ya jamii kwa sasa.
7. Je, ni kwa namna gani muziki unaweza kutumika kukuza
maadili ya jamii kwa sasa?
149
06/11/2024 11:30:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 149
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 149 06/11/2024 11:30:25