Page 153 - Historiayatznamaadili
P. 153
Kazi ya kufanya namba 7
Fanya uchunguzi kuhusu maana ya ngoma
zinazochezwa katika jamii yako ukizingatia midundo
na maneno ya nyimbo hizo na nafasi yake katika
FOR ONLINE READING ONLY
kukuza na kutunza maadili.
Misingi ya mamlaka za jadi katika ukuzaji na utunzaji wa
maadili
Mamlaka za jadi zilisimamia misingi mbalimbali katika ukuzaji
na utunzaji wa maadili. Misingi hiyo ni kama ifuatavyo:
(a) Heshima. Utunzaji na ukuzaji wa maadili ulisimamiwa
katika misingi ya heshima. Mamlaka za jadi na jamii
nzima ziliheshimu misingi ya maadili iliyokuwapo katika
jamii. Mamlaka za jadi zilifuata sheria, mila na desturi
walizorithishwa na mababu na mabibi zao. Mamlaka za
jadi zilisimamia na kuhakikisha kila mwanajamii anazifuata.
Pale, ilipotokea ukiukwaji wa maadili, viongozi walichukua
hatua za kinidhamu dhidi ya wahusika ili kukuza na kutunza
maadili ya jamii zao.
Zoezi namba 4
1. Eleza umuhimu wa viongozi kuendelea kuheshimu
maadili ya jamii katika ukuzaji na utunzaji wa maadili ya
jamii kwa sasa.
2. Eleza hasara za kutokuhesimu maadili ya jamii katika
kukuza na kutunza maadili.
(b) Uadilifu. Uadilifu uliheshimiwa katika ukuzaji na utunzaji
wa maadili. Usimamizi wa maadili ulifanyika katika misingi
ya uwazi, ukweli na haki kwa watu wote. Hapakuwa na
upendeleo katika utoaji wa adhabu na kukemea vitendo
vilivyokuwa kinyume na maadili. Kila mtu alipewa onyo na
146
06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 146
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 146 06/11/2024 11:30:24