Page 155 - Historiayatznamaadili
P. 155
walimu, na watu wengine katika jamii inayomzunguka.
Hivyo, mtoto anapaswa kuwa msikivu ili kujifunza maadili
ya jamii yake na kutoka kwa viongozi waliopo;
(b) Kutii sheria, kanuni na taratibu za jamii yake. Utii wa
FOR ONLINE READING ONLY
sheria na kanuni utamwezesha mtoto kuishi kulingana na
mila na desturi za familia, ukoo, jamii na Taifa kwa ujumla.
Pia, utamwezesha mtoto kuishi kwa amani katika jamii
inayomzunguka;
(c) Kulinda na kudumisha maadili ya jamii yake. Mtoto
anaweza kulinda maadili ya jamii kwa kuacha vitendo
vilivyo kinyume na maadili. Pia, mtoto anapaswa kukemea
vitendo vilivyo kinyume na maadili vinavyotendwa na watoto
wenzake na wanajamii. Mtoto anaweza kukemea kwa
kupinga na kukataa kushiriki vitendo hivyo;
(d) Kuripoti vitendo vilivyo kinyume na maadili. Mtoto anao
wajibu wa kutoa taarifa zinazohusu ukiukwaji wa maadili.
Mfano, anaweza kutoa taarifa kwa wazazi, walezi, walimu
na serikali za Mtaa/Kijiji. Pia, anaweza kutoa taarifa katika
mamlaka za kisheria kama vile, polisi, Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa na Mamlaka ya Kudhibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya. Mtoto hapaswi kukaa
kimya au kuficha anapofanyiwa vitendo viovu na anapoona
vinafanyika; na
(e) Kuelimisha. Mtoto anaweza kuwaelimisha watoto wenzake
na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kukuza na kutunza
maadili.
Kazi ya kufanya namba 10
Jadili na kuandika mikakati ya kutoa elimu ya kukuza
na kutunza maadili katika jamii.
148
06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 148 06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 148