Page 150 - Historiayatznamaadili
P. 150
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1: Michoro ya mapangoni
(ii) Muziki na nyimbo. Nyimbo zenye maudhui ya kukuza
na kutunza maadili ziliimbwa na kuchezwa katika
matukio ya kijamii. Kwa mfano, nyimbo zilizoimbwa
wakati wa harusi, zilieleza wanandoa namna ya kuishi
katika ndoa. Nyimbo zilizoimbwa wakati wa kulima na
mavuno zilieleza maadili katika kilimo. Vivyo hivyo,
nyimbo zilizoimbwa wakati wa kuzaliwa mtoto zililenga
malezi ya mtoto. Kila tukio lilikuwa na nyimbo zake na
zenye mafundisho ya kimaadili. Watu waliokiuka maadili
walitungiwa nyimbo za kuonya. Hii ilisababisha watu
kuzingatia maadili.
Kazi ya kufanya namba 5
Jadili nafasi chanya na hasi za muziki wa kizazi kipya
katika kukuza na kutunza maadili ya jamii nchini kwa
sasa.
143
06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 143 06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 143