Page 148 - Historiayatznamaadili
P. 148
(b) Kuonya kwa kukemea uvunjaji wa maadili ya jamii.
Yeyote aliyekiuka maadili ya jamii alipewa adhabu kali.
Baadhi ya adhabu zilitolewa mbele ya jamii nzima. Hii
ilisaidia watu kutambua athari za ukiukaji wa maadili katika
jamii.
FOR ONLINE READING ONLY
(c) Vitisho. Vitisho vilikuwa njia mojawapo katika kukuza na
kutunza maadili. Vitisho vilitolewa vikiambatana na miiko
yenye mila na desturi ili kuifanya jamii kuogopa madhara
ya ukiukaji wa maadili. Miiko iliwekwa na ilisimamiwa na
mamlaka za jadi ili kukuza na kutunza maadili.
Zoezi namba 2
1. Andika miiko mitatu (3) iliyotumika kukuza na kutuza
maadili.
2. Fafanua maana ya miiko ifuatayo:
(i) Usisimulie hadithi mchana utaota mkia.
(ii) Usishone nguo ukiwa umevaa, utakuwa maskini.
(iii) Usipige mluzi usiku, utamwita shetani.
(iv) Usifagie usiku, utafukuza bahati.
(v) Usimpige mwenzio kwa ufagio.
3. Eleza umuhimu wa matumizi ya miiko katika kukuza na
kutunza maadili.
(d) Elimu. Elimu ilitumika kama njia ya kukuza na kutunza
maadili. Watoto wadogo walifundishwa maadili na watu
wazima, ikiwemo wazazi wao. Pia, elimu za unyago na
jando zilitumika kukuza na kutunza maadili ya jamii. Pamoja
na kuwapo watu rasmi wa kutoa elimu za jando na unyago,
mamlaka za jadi zilisimamia ili kuhakikisha utekelezaji
wake katika jamii nzima. Elimu hii ilikuwa ya lazima kwa
kila mwanajamii. Maarifa na stadi zilizotolewa zilisaidia
141
06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 141 06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 141