Page 144 - Historiayatznamaadili
P. 144
Sura ya Mamlaka za jadi katika ukuzaji
Saba na utunzaji wa maadili
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Jamii zetu zilikuwa na mifumo ya ukuzaji na utunzaji wa maadili. Katika
sura hii, utajifunza mchango wa mamlaka za jadi katika ukuzaji na utunzaji
wa maadili katika jamii kabla ya ukoloni. Pia, utajifunza wajibu wa mtoto
katika ukuzaji na utunzaji wa maadili ya jamii. Umahiri utakaoupata
utakusaidia kutambua mchango wa mamlaka za jadi katika ukuzaji na
utunzaji wa maadili. Hivyo, kuthamini mifumo iliyopo katika kukuza na
kutunza maadili katika jamii.
Fikiri
Mchango wa mamlaka za jadi katika ukuzaji na
utunzaji wa maadili kabla ya ukoloni.
Mifumo ya ukuzaji na utunzaji wa maadili
Kazi ya kufanya namba 1
Jadili namna maadili yanavyosimamiwa katika jamii
yako.
Jamii zilikuwa na mifumo maalumu ambayo ilisimamia maadili
ya jamii. Mifumo hii ya usimamizi ilikuwapo tangu ngazi ya
familia, ukoo mpaka jamii. Mifumo hii ilisimamia misingi,
kanuni na taratibu za kisheria zilizoonesha namna ambavyo
maadili yalipaswa kufanyika kwa usahihi na ufanisi katika ngazi
husika. Usimamizi wa maadili ulijikita katika kuhakikisha jamii
137
06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 137 06/11/2024 11:30:22
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 137