Page 146 - Historiayatznamaadili
P. 146
Mamlaka za jadi katika ukuzaji na utunzaji maadili
Kazi ya kufanya namba 3
Fanya uchunguzi kuhusu namna mamlaka za jadi
FOR ONLINE READING ONLY
zilivyosimamia ukuzaji na utunzaji wa maadili katika
jamii yako.
Mamlaka za jadi zilikuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji
na utunzaji wa maadili. Mamlaka za jadi zilisimamia ukuzaji na
utunzaji wa maadili katika jamii. Aidha, mamlaka hizo zilikuwa
ndiyo ngazi ya mwisho ya usimamizi wa maadili katika jamii.
Mamlaka za jadi zilikuwa na majukumu yafuatayo katika kukuza
na kutunza maadili yao.
(a) Kutunga sheria, kanuni na taratibu za jamii. Mamlaka
za jadi zilisimamia utungaji wa sheria, kanuni na taratibu
za jamii. Hii ilisaidia jamii zao kuwa na sheria, kanuni na
taratibu zilizotambuliwa na jamii nzima. Hivyo, ilikuwa
wajibu kisheria kwa jamii nzima kuzingatia mila na desturi
zilizokubalika katika jamii. Aidha, mamlaka hizi zilikuwa
na wajibu wa kubadilisha sheria au kanuni zisizofaa au
ambazo zimepitwa na wakati, hazina tija, haziendani na
mazingira au hazikukidhi matakwa ya jamii zao. Hii ilisaidia
kukuza maadili yaliyoendana na wakati katika jamii zao.
(b) Kusimamia maadili ya jamii. Mamlaka za jadi ndizo
zilizosimamia ukuzaji na utunzaji wa maadili. Jambo la
kimaadili liliposhindikana katika ngazi za chini, lilipelekwa
katika mamlaka hizo kwa utatuzi. Mamlaka za jadi zilikuwa
na maamuzi ya juu.
(c) Kusimamia shughuli za kimila, kama vile ibada,
matambiko na dini za jadi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa
mamlaka hizi zilikuwa na watu wenye nguvu za miungu ya
kabila. Hii ilisaidia jamii nzima kuthamini mila na desturi
zao na kuzifuata.
139
06/11/2024 11:30:23
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 139
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 139 06/11/2024 11:30:23