Page 152 - Historiayatznamaadili
P. 152
Kazi ya kufanya namba 6
Jadili nafasi chanya na hasi za tamthilia na michezo
ya kuigiza katika kukuza na kutunza maadili ya jamii
kwa sasa.
FOR ONLINE READING ONLY
(v) Ususi. Ususi ulitumika kukuza na kutunza maadili.
Wasusi walisuka vitu na kuandika maandishi yenye
kusisitiza mila na desturi
za jamii. Mfano, maneno
kama “umoja ni nguvu”,
yalitumika kusisitiza
upendo, umoja na
ushirikiano. Kielelezo
namba 3, kinaonesha
mapambo yenye kutoa Kielelezo namba 3: Kawa lenye
ujumbe wa kusisitiza ujumbe wenye maadili
maadili.
(vi) Ngoma. Jamii zilikuwa na ngoma tofauti, mfano ngoma
za sindimba, mdundiko, msewe, mganda, muheme,
bugobogobo, ligombe na kadhalika. Ngoma hizi
ziliambatana na nyimbo na dansi zenye kufunza mila
na desturi za jamii. Ngoma mbalimbali zilichezwa wakati
tofauti ili kuelezea maadili husika. Ngoma za wakati wa
sherehe za jando, unyago, harusi, masika, au mavuno
zilitofautiana kwa midundo na dansi. Kadiri ngoma
zilivyochezwa, ndivyo jamii ilivyojikumbusha maadili
ya jamii zao. Viongozi wa jadi walikuwapo kusimamia
maadili katika sherehe hizo.
145
06/11/2024 11:30:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 145
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 145 06/11/2024 11:30:24