Page 160 - Historiayatznamaadili
P. 160
Kazi ya kufanya namba 2
Fanya uchunguzi wa Nembo ya Taifa, kisha andika
vitu vilivyopo katika nembo hiyo.
FOR ONLINE READING ONLY
Nembo ya Taifa ina alama mbalimbali kama vile bibi na bwana,
mwenge, bendera ya Taifa, jembe na nyundo, milia ya bluu,
pembe za ndovu, mlima, mkuki, karafuu, pamba, rangi ya
dhahabu (njano) na maneno “uhuru na umoja”.
Kazi ya kufanya namba 3
Jadili na andika maana ya alama zilizopo katika
nembo ya Taifa.
Alama zilizopo katika nembo ya Taifa zina maana mahususi
katika utambulisho wa historia ya Taifa la Tanzania. Alama hizi
zina utambulisho wa watu, historia ya nchi na rasilimali zilizopo
nchini. Mfano, alama ya Bendera ya Taifa inaashiria uhuru wa
Taifa letu. Alama ya watu wawili; mtu mume na mke ambao
wameshika ngao ni ishara ya kusisitiza usawa na ushirikiano
wa jinsi zote katika jamii yetu ya Kitanzania. Alama ya mlima,
ni ishara ya uwepo wa mlima mrefu wa Kilimanjaro, ambao ni
fahari kwa nchi ya Tanzania. Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu
kuliko yote barani Afrika. Pamba na karafuu huwakilisha mazao
muhimu ya biashara yanayopatikana katika nchi yetu. Alama
ya mwenge ni kiashirio cha ishara ya uhuru wetu. Mwenge huu
uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya mlima Kilimanjaro wakati
nchi ilipopata uhuru.
Rangi ya njano (dhahabu) ni alama inayoashiria uwepo wa
rasilimali za madini ya dhahabu nchini. Alama ya jembe na
shoka husisitiza umuhimu wa kazi kama msingi wa ujenzi wa
maisha ya Mtanzania. Alama ya mkuki na ngao vinawakilisha
153
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 153 06/11/2024 11:30:25
06/11/2024 11:30:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 153