Page 163 - Historiayatznamaadili
P. 163
Kazi ya kufanya namba 5
Imba Wimbo wa Taifa.
FOR ONLINE READING ONLY
Mwenge wa Uhuru
Mwenge wa Uhuru umebeba alama ya uhuru wa Taifa la
Tanzania. Mwenge huu kwa mara ya kwanza uliwashwa na raisi
wa kwanza nchini, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
mwaka 1961; Tanganyika ilipopata uhuru. Mwenge huu
uliwashwa kuashiria mwanga nchini, na kama alama ya kuondoa
utawala wa kikoloni nchini. Ukoloni ulionekana kama ni kiza
kikuu ndani ya nchi. Hii ni kwa sababu, nchi ilikuwa haina uhuru
wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Watanzania walilazimishwa
kufuata siasa na mila na desturi za wakoloni na hivyo, kupoteza
uhuru na utu wao. Mwenge hutambulika kama Mwenge wa
Uhuru, kwa sababu uliwashwa kuonesha nuru mpya ya mafanikio
na uhuru wa Mtanzania baada ya kuondoa ukoloni nchini.
Kielelezo namba 4, kinaonesha mwenge wa uhuru.
Mwaka 1964, mwenge wa uhuru
ulianza kukimbizwa nchi nzima,
na hadi sasa hukimbizwa kama
alama ya matumaini mapya nchini
yaliyoletwa na uhuru. Mwenge
huu kila uwashwapo hukumbusha
Watanzania umuhimu wa ujasiri wa
kutenda mambo kisiasa, kiuchumi
kulingana na maadili ya Kitanzania
baada ya kuondoa ubaguzi,
unyanyasaji na ukandamizaji
uliofanywa na wakoloni nchini. Kielelezo namba 4:
Mwenge wa Uhuru
156
06/11/2024 11:30:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 156
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 156 06/11/2024 11:30:25