Page 168 - Historiayatznamaadili
P. 168
Alama za Taifa ni alama muhimu katika utambulisho wa Taifa.
Alama hizi zinapaswa kuheshimiwa na kutumika kwa usahihi
kulitambulisha Taifa letu. Kuheshimu alama za Taifa ni kitendo
cha uzalendo.
FOR ONLINE READING ONLY
Zoezi la jumla
1. Taja alama za Taifa____________
2. Kuna umuhimu gani wa kuwa na alama za Taifa kwa nchi?
3. Je, kuna umuhimu gani wa kuheshimu alama za Taifa?
4. Eleza umuhimu wa sikukuu za Kitaifa nchini.
5. Fafanua maana ya rangi zilizopo katika Bendera ya Taifa.
6. Andika hatua utakazochukuwa iwapo:
(i) Utapita eneo ambalo Bendera ya Taifa inashushwa
muda huo;
(ii) Wimbo wa Taifa unaimbwa;
(iii) Utakutana na watu wanachana fedha za Taifa;
(iv) Utaalikwa kwenye sherehe za kimataifa na utahitajika
kubeba alama ya utambulisho wa Taifa lako; na
(v) Mwenge wa Uhuru utawashwa katika eneo unaloishi.
161
06/11/2024 11:30:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 161 06/11/2024 11:30:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 161