Page 166 - Historiayatznamaadili
P. 166
Kazi ya kufanya namba 8
Chunguza noti ya shilingi 10,000, 5,000 na 2,000
na sarafu ya shilingi 500, 200 na 100 kisha andika
alama zilizopo.
FOR ONLINE READING ONLY
Fedha za Tanzania zina alama zenye viongozi wakuu wa nchi
na rasilimali zilizopo nchini. Fedha zinapaswa kuheshimiwa
katika matumizi na kwa ajili ya ustawi wa mtu binafsi, jamii na
Taifa kwa ujumla. Fedha hutumika kwa ajili ya kupata huduma
kama vile chakula, malazi, mavazi, elimu na mahitaji mengine
ya jamii. Hivyo, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kutokuheshimu
fedha hizi, kutupa, kuchana au kuchafua fedha kwa makusudi.
Sikukuu za Kitaifa
Sikukuu za Kitaifa ni alama muhimu zilizobeba utambulisho
wa Taifa la Tanzania. Sikukuu hizi ni zile zenye matukio yenye
kuonesha kumbukumbu za kihistoria nchini.
Kazi ya kufanya namba 9
Jadili na andika sikukuu za Kitaifa nchini na
kumbukumbu zilizoambana nazo.
Sikukuu za Kitaifa hutambulika nchini na huadhimishwa kila
mwaka. Orodha ifuatayo inaonesha sikukuu za kitaifa nchini:
(a) 9 Disemba. Hii ni sikukuu ya kitaifa, yenye kumbukizi
ya kihistoria, ambapo nchi ya Tanganyika ilipata uhuru;
(b) 12 Januari, ni sikukuu ya kitaifa, yenye kumbukizi ya
kihistoria, ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar yalipofanyika.
Mapinduzi haya yalifanyika ili kuondoa utawala wa
kisultani na kuweka utawala wa Wazanzibari. Mapinduzi
haya yalikuwa ni muhimu katika kupata uhuru rasmi.
Wazanzibari hawakuwa na uhuru kamili, kwa sababu nchi
hii ilipopewa uhuru, madaraka yalibaki kwa sultani; na
159
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 159 06/11/2024 11:30:26
06/11/2024 11:30:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 159