Page 162 - Historiayatznamaadili
P. 162

Rangi ya njano inawakilisha uwapo wa rasilimali za madini nchini.
              Kimsingi alama ya bendera ni utambulisho wa Taifa huru, watu
              wake, maliasili zilizopo na utajiri wa nchi ya Tanzania.


              Wimbo wa Taifa la Tanzania
          FOR ONLINE READING ONLY
              Wimbo wa Taifa ni alama inayotambulisha Taifa la Tanzania.

              Kielelezo namba 3, kinaonesha wimbo wa Taifa.

                Mungu Ibariki Afrika,                Wimbo huu huimbwa katika

                Wabariki Viongozi Wake,              matukio muhimu ya Kitaifa
                Hekima, Umoja na Amani,              ndani  na  nje  ya  mipaka  ya
                Hizi ni Ngao Zetu,                   Tanzania. Matukio hayo ni
                Afrika na Watu Wake.                 pamoja na: Rais akihutubia
                Ibariki, Afrika,                     Taifa, Rais akihutubia Bunge,
                Ibariki, Afrika,                     misiba ya Kitaifa, matukio
                Tubariki Watoto wa Afrika.           ya Kitaifa kama michezo na

                                                     ziara za Kitaifa zinazohusisha
                Mungu Ibariki Tanzania,
                Dumisha Uhuru na Umoja,              viongozi wakuu wa nchi na nje
                Wake kwa Waume na                    ya nchi.
                Watoto,                              Wimbo huu huimbwa kwa ajili
                Mungu Ibariki,                       ya kuiombea nchi ya Tanzania
                Tanzania na Watu Wake,               na Bara la Afrika baraka na
                Ibariki, Tanzania,                   amani. Pia, unasisitiza uwepo

                Ibariki, Tanzania,                   wa amani, upendo na umoja
                Tubariki, Watoto wa                  kwa watu wa Tanzania, bila
                Tanzania.                            ya kujali jinsi, rangi wala hali

                      Kielelezo namba 3:             ya mtu.
                        Wimbo wa Taifa

              Wimbo huu unapoimbwa kila mtu anapaswa kusimama wima
              na kutulia. Hii hufanyika ili kuonesha heshima na nidhamu kwa

              wimbo huu wa Taifa, kwa sababu ni alama kuu ya Taifa. Wimbo
              huu hutumika kwa matukio rasmi ya Kitaifa. Ni marufuku kutumia
              wimbo wa Taifa kwa matumizi yasiyo rasmi.




                                                   155




                                                                                          06/11/2024   11:30:25
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   155
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   155                                    06/11/2024   11:30:25
   157   158   159   160   161   162   163   164   165   166   167