Page 164 - Historiayatznamaadili
P. 164
Kazi ya kufanya namba 6
Chunguza, kisha andika shughuli zinazoambatana
na tukio la mwenge wa uhuru katika eneo
linalokuzunguka.
FOR ONLINE READING ONLY
Mnyama twiga
Mnyama Twiga ni alama ya utambulisho wa Taifa. Alama hii
ni kiashirio cha uwepo wa mbuga zenye wanyama mbalimbali
nchini Tanzania. Twiga ni mnyama anayeashiria amani licha ya
ukubwa wake. Tanzania ina mbuga za wanyama zenye wanyama
wa aina tofauti. Kielelezo namba 5, kinaonesha picha ya Twiga.
Mbuga za wanyama ni fahari ya nchi yetu. Tanzania ina mbuga
za wanyama kama vile,
Ngorongoro, Manyara, Mikumi,
Tarangire, Ruaha, Serengeti,
Jozani (Unguja), Ngezi
(Pemba), Rubondo na Saanane.
Licha ya mbuga hizi kuna
mapori tengefu mengi. Mfano,
takribani asilimia 28 ya maeneo
ya ardhi nchini yamehifadhiwa
kwa ajili ya mbuga na hifadhi za
Kielelezo namba 5:
Mnyama Twiga wanyamapori.
Kazi ya kufanya namba 7
Andika orodha ya wanyamapori wanaopatikana
nchini Tanzania.
Watalii wengi huja kutembelea mbuga hizi kwa ajili ya kuona
wanyama. Watalii hawa hulipatia Taifa fedha za kigeni. Hivyo,
kuinua pato la Taifa.
157
06/11/2024 11:30:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 157
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 157 06/11/2024 11:30:26