Page 167 - Historiayatznamaadili
P. 167
(c) 26 Aprili, ni sikukuu ya kitaifa yenye kumbukizi ya
kihistoria ambapo Tanganyika na Zanzibar ziliungana
na kuzaliwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
FOR ONLINE READING ONLY
Sikukuu hizi ndizo muhimu kwa historia ya Mtanzania katika
kupata uhuru na kuwa Taifa huru. Pia, zipo sikukuu zingine za
kitaifa kama siku za wafanyakazi (Mei mosi), wafanyabiashara
(Sabasaba) na wakulima (Nanenane).
Matumizi ya alama za Taifa
Alama za Taifa ni muhimu katika utambulisho wa Taifa la
Tanzania. Hivyo, alama hizo hutumika katika shughuli za kitaifa
na nyaraka za kitaifa.
Kazi ya kufanya namba 10
Jadili matumizi ya alama za Taifa.
Alama za Taifa hutumika katika maeneo kadhaa kutambulisha
nchi ya Tanzania. Kwa mfano, nembo ya Taifa, huwekwa katika
nyaraka muhimu za nchi ili kuzitambulisha kuwa ni mali ya Taifa
na siyo mali ya mtu binafsi. Nembo hii hutumika pia katika
barua za kiserikali ili kuitambulisha serikali. Nembo hii huashiria
umuhimu wa nyaraka husika kwa Taifa.
Pia, bendera ya Tanzania hutumika katika ofisi za serikali,
mikutano na ziara za kiserikali ili kulitambulisha Taifa la Tanzania.
Kila watu waonapo bendera hii hutambua uwapo wa Taifa la
Tanzania. Aidha, fedha za Tanzania, hutumika kama alama ya
kuhalalisha matumizi ya fedha husika katika shughuli mbalimbali.
160
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 160 06/11/2024 11:30:26
06/11/2024 11:30:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 160