Page 165 - Historiayatznamaadili
P. 165
Fedha ya Tanzania
Fedha ni alama muhimu inayolitambulisha Taifa letu. Mara
baada ya kupata uhuru, Tanzania ilianza kutumia fedha zake.
Fedha hizi zipo katika sarafu na noti. Aidha, fedha hizi zina alama
FOR ONLINE READING ONLY
kadhaa kwa ajili ya utambulisho wa historia ya nchi na rasilimali
zilizopo. Kielelezo namba 6, kinaonesha baadhi ya sarafu na noti
zilizotumika awali nchini.
Kielelezo namba 6: Sarafu na noti zilizotumika zamani nchini
Aidha, tangu nchi ipate uhuru kumekuwa na mabadiliko ya
sarafu na noti zinazotumika nchini. Hii inatokana na mabadiliko
ya uchumi yanayotokea mara kwa mara nchini. Kwa sasa, fedha
za Tanzania ni tofauti na zilizopo katika kielelezo namba 6.
Kielelezo namba 7, kinaonesha fedha zinazotumika kwa sasa.
Kielelezo namba 7: Sarafu na noti za fedha zinazotumika sasa
158
06/11/2024 11:30:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 158 06/11/2024 11:30:26
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 158