Page 161 - Historiayatznamaadili
P. 161
silaha za jadi za ulinzi kama nyenzo za ulinzi nchini. Milia ya
bluu inawakilisha rasilimali za maji kama vile bahari, mito na
maziwa nchini. Alama ya pembe za ndovu inaonesha uwapo wa
utajiri mkubwa wa wanyama katika nchi ya Tanzania. Maneno
FOR ONLINE READING ONLY
“UHURU NA UMOJA” ni alama inayosisitiza uhuru na umoja wa
watu wa Tanzania.
Nembo ya Taifa ina alama zenye utambulisho wa rasilimali za
Taifa, matukio ya Kihistoria, utajiri wa Taifa letu na maadili ya
Taifa. Kimsingi, Nembo ya Taifa hutoa utambulisho wa Taifa
ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina alama zenye
utambulisho wa Taifa.
Kazi ya kufanya namba 4
Chunguza bendera ya Taifa, kisha andika maana ya
rangi zilizopo katika bendera hiyo.
Bendera ya Taifa ni alama ya utambulisho wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kama Taifa huru. Kielelezo namba 2,
kinaonesha Bendera ya Taifa.
Bendera ina rangi nne ambazo
zinatambulisha Taifa letu. Rangi
nyeusi inawakilisha alama ya
uwepo wa watu wenye asili
ya Kiafrika. Rangi ya kijani
inawakilisha ardhi na uoto wa
asili. Rangi ya bluu (samawati)
inawakilisha utajiri wa maji:
bahari, maziwa na mito iliyopo
Kielelezo namba 2: ndani ya nchi na inayolizunguka
Bendera ya Taifa Taifa la Tanzania.
154
06/11/2024 11:30:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 154 06/11/2024 11:30:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 154