Page 158 - Historiayatznamaadili
P. 158
Sura ya Alama za Taifa na
Nane utambulisho wa Taifa
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Taifa lina alama mbalimbali zitumikazo katika kujitambulisha. Katika
sura hii utajifunza kuhusu alama za Taifa na utambulisho wake katika
Taifa. Umahiri utakaoupata utakuwezesha kuthamini alama za Taifa na
matumizi yake katika utambulisho wa Taifa. Aidha, kuzitambua alama za
Taifa kutakujengea misingi ya uzalendo. Hivyo, kulinda na kuthamini Taifa
na rasilimali zake.
Fikiri
Umuhimu wa alama za Taifa katika utambullisho
wa Taifa.
Alama za Taifa
Alama ni kitu chochote kinachosimama kama ishara yenye
maana ya ziada katika kuwasilisha jambo. Alama ni utambullisho,
ambao hutambulisha kitu, kundi la watu, jamii au Taifa. Alama
mara nyingi hutofautiana ili kutambulisha vitu tofauti. Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina alama zinazosimama
na kutoa utambulisho wake. Alama hizi zinaonesha historia
ya matukio, rasilimali zilizopo (kama bahari, milima, wanyama,
dhahabu na kadhalika) na shughuli za jamii. Alama hizi
zimebeba misingi ya utamaduni wa Mtanzania. Kimsingi, alama
za Taifa zinawakilisha umoja na fahari ya serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
151
06/11/2024 11:30:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 151
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 151 06/11/2024 11:30:25