Page 103 - Historiayatznamaadili
P. 103
Zoezi namba 6
1. Ainisha maadili yaliyozingatiwa katika shughuli za uchumi
ili kutunza afya ya jamii.
FOR ONLINE READING ONLY
2. Fafanua umuhimu wa maadili katika shughuli za uchumi
katika kutunza afya ya jamii.
Matumizi ya mifumo ya imani za jadi
Maadili katika shughuli za uchumi yalitumia mifumo ya imani za
jadi. Mfano, ibada zilizohusisha matambiko maalumu zilifanyika
kabla ya kuanza shughuli za uchumi. Ibada zilifanyika kwa lengo
la kuomba baraka katika utendekaji wa kazi na kuomba mavuno
mengi. Pia, ibada zilifanyika kuondoa vikwazo katika shughuli
za uchumi. Mfano, jamii za wahunzi zilifanya ibada ili kutakasa
rasilimali watu na vifaa katika shughuli za uhunzi. Vilevile, ibada
zilifanyika baada ya shughuli za uchumi ili kuishukuru miungu
kwa kupata mavuno mengi. Baadhi ya jamii, zilitoa mavuno ya
kwanza kama sadaka ya miungu wao.
Maadili katika kazi
Maadili katika shughuli za uchumi yalizingatia jinsi. Palikuwapo
na kazi zilizofanywa na wanawake na zile za wanaume. Mipaka
iliwekwa katika jinsi kwa ajili ya ustawi wa jamii na usalama.
Wanawake hawakuhusishwa katika baadhi ya shughuli kwa
ajili ya ulezi wa watoto na familia. Baadhi ya shughuli kama vile
uhunzi, uwindaji na ufugaji zilihitaji kutembea na kukaa porini
muda fulani. Hali hii ilionekana kuwa ngumu kwa wanawake
kwa sababu ya ulezi wa familia na watoto.
Maadili katika jamii pia yalisisitiza kila mwanajamii kufanya kazi
ili kuendeleza shughuli za uchumi katika jamii zao. Watu ambao
hawakufanya kazi walikuwa ni wazee, watoto na wagonjwa.
Jamii zilithamini kazi; kazi ilikuwa kipimo cha utu. Pia, jamii
zilifanya shughuli za uchumi kwa kushirikiana ambapo wanajamii
96
06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 96
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 96 06/11/2024 11:30:15