Page 100 - Historiayatznamaadili
P. 100
Hii ilisababisha shughuli za uchumi kukua ili kukidhi mahitaji ya
jamii.
Shughuli za uchumi zilisaidia kukua kwa shughuli zingine
za uchumi. Mfano,viwanda vya zana za chuma viliwezesha
FOR ONLINE READING ONLY
wakulima kulima eneo kubwa zaidi. Hivyo, kupata chakula cha
kutosha kulisha jamii zao na kuwa na ziada. Pia, viwanda hivi
vilisaidia kukua kwa shughuli za uvuvi, uchongaji na uwindaji.
Vilevile,viwanda vya ususi, chumvi na uchongaji vilisaidia kukua
kwa shughuli za uvuvi. Aidha, shughuli za uchumi zilichangia
kukua kwa shughuli za biashara.Jamii zilibadilishana ziada ili
kupata vitu vingine kutoka jamii zingine. Vivyo hivyo, wafugaji
walibadilishana maziwa na mifugo kwa nafaka kutoka kwa
wakulima. Wavuvi walibadilishana samaki ili kupata nafaka
kutoka kwa wakulima. Hii iliimarisha biashara kati ya jamii na
jamii. Shughuli za uchumi zilizisaidia jamii kukidhi mahitaji yao
kabla ya kuja kwa ukoloni.
Shughuli za uchumi zilisababisha jamii za kale kujenga makazi
ya kudumu. Kuimarika kwa makazi kulisababisha kukua na
kuimarika kwa mamlaka za jadi. Kwa ujumla, shughuli za uchumi
zilichangia kukua kwa shughuli nyingine za uchumi, kuimarika
kwa makazi ya jamii, kukua kwa mamlaka za jadi na kukuza
uhusiano kati ya jamii. Hivyo kuleta maendeleo kabla ya kuja
kwa wakoloni nchini.
Maadili katika shughuli za uchumi
Kazi ya kufanya namba 11
Fanya uchunguzi kuhusu shughuli za uchumi
zinazofanyika katika eneo linalokuzunguka, kisha
andika maadili yake.
Maadili katika shughuli za uchumi yalilenga katika kulinda
rasilimali asilia za uchumi, kuomba baraka za mavuno, kutunza
afya ya jamii, kujenga ushirikiano na uhusiano katika kazi na
uhifadhi wa maarifa na ujuzi wa jamii husika. Jamii zilitambua
93
06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 93
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 93 06/11/2024 11:30:15