Page 98 - Historiayatznamaadili
P. 98
Bidhaa za uchongaji zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya jamii na
kwa ajili ya biashara ili kupata bidhaa ambazo hazikuwapo katika
jamii zao.
Kazi ya kufanya namba 8
FOR ONLINE READING ONLY
Fanya uchunguzi kwa kuuliza, kusoma matini au
kutembelea maeneo yenye shughuli za uchumi za
uchongaji, kisha eleza namna jamii inavyoziendeleza
kwa sasa.
Shughuli za uchumi katika uchongaji zilikuwapo kabla ya ujio
wa wakoloni nchini. Shughuli za uchumi katika uchongaji bado
zinaendelea katika jamii zetu mpaka sasa. Watalii hupendelea
kununua vitu vya kuchongwa kwa ajili ya mapambo na matumizi
mengine ya nyumbani hadi sasa.
Mzee Kukawa alihitimisha simulizi na wageni wote walishangilia
kwa nderemo na vifijo.
Kazi ya kufanya namba 9
Andika jinsi ya kuendeleza shughuli za uchumi katika
uchongaji kwa maendeleo ya uchumi na jamii kwa
sasa.
Shughuli za uchumi za utengenezaji wa chumvi
Mzee aliyefuata alikuwa Mzee Kware kutoka maeneo ya Uvinza,
mkoa wa Kigoma. Mzee huyu aliwakilisha shughuli za uchumi za
utengenezaji chumvi. Mzee Kware alianza kwa kuelezea kuwa:
Shughuli za utengenezaji chumvi zilikuwa shughuli kuu ya uchumi
kwa jamii zilizoishi maeneo yenye maji yenye asili ya chumvi.
Mfano, wa jamii hizo ni za Uvinza huko Kigoma zinazoishi kando
ya mto Malagarasi. Jamii zingine ni zile zinazoishi Ivuna, Rukwa,
Ziwa Eyasi, Ziwa Balangida na Kitangiri.
91
06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 91
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 91 06/11/2024 11:30:15