Page 99 - Historiayatznamaadili
P. 99
Shughuli za utengenezaji wa chumvi zilifanyika kwa ajili ya kukidhi
mahitaji ya jamii na biashara. Mfano, chumvi iliyotengenezwa
Uvinza ilikuwa bidhaa muhimu sana wakati wa biashara za jamii
na zile za masafa marefu. Jamii hizo zilibadilishana chumvi na
jamii zilizowazunguka na zile za mbali ili kupata bidhaa zingine.
FOR ONLINE READING ONLY
Wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali walihitaji chumvi ili
kubadilishana na chakula wakiwa njiani. Karibu kila jamii ilihitaji
chumvi kama ilivyohitaji zana za chuma.
Kazi ya kufanya namba 10
Andika jinsi ya kuendeleza shughuli ya utengenezaji
chumvi kwa maendeleo ya uchumi na jamii kwa sasa.
Mzee Kware alihitimisha huku watu wote wakimpigia makofi na
vifijo.
Zoezi namba 4
1. Eleza mchango wa viwanda vya ususi katika maendeleo
ya uvuvi kabla ya ukoloni.
2. Fafanua namna viwanda vya uchongaji vilivyosaidia
maendeleo ya uvuvi kabla ya ukoloni.
3. Ni kwa namna gani matumizi ya moto na chumvi
yalivyosaidia kukua kwa uvuvi nchini kabla ya ukoloni?
Mchango wa shughuli za uchumi katika maendeleo ya jamii
Shughuli za uchumi zilikuwa na mchango mkubwa katika
maendeleo ya jamii kabla ya ukoloni. Shughuli za uchumi
katika jamii zilitegemeana ili kukidhi mahitaji yake. Mfano, jamii
zilizotengeneza chumvi zilitegemea wakulima ili kupata chakula.
Pia, wakulima walitegemea jamii za wahunzi ili kupata majembe,
mashoka, mapanga na zana nyinginezo kwa ajili ya shughuli za
kilimo. Aidha, viwanda vya uchongaji vilitegemea viwanda vya
uhunzi na viwanda vya ususi vilitegemea wakulima na kadhalika.
92
06/11/2024 11:30:15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 92
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 92 06/11/2024 11:30:15