Page 91 - Historiayatznamaadili
P. 91
Shughuli za uvuvi zilifanywa na jamii za watu walioishi maeneo ya
Pwani ya Bahari ya Hindi. Pia, zilifanyika katika maeneo ya bara
yenye maziwa makubwa kama vile ziwa Victoria, Tanganyika,
na Nyasa. Vilevile, uvuvi ulifanyika katika mito mikubwa kama
FOR ONLINE READING ONLY
vile mto Rufiji, Ruvuma, Malagarasi na Pangani. Jamii zilizoishi
maeneo ya mwambao wa bahari na ziwa ndizo zilizovua samaki
kwa wingi zaidi.
Kazi ya kufanya namba 3
Chunguza ramani ya Tanzania, kisha onesha
maeneo yenye bahari, mito na maziwa yaliyohusika
na shughuli za uvuvi.
Shughuli za uchumi za uvuvi zilifanyika kwa kutumia nyavu za asili
na mitego mbalimbali. Nyavu zilizotumika zilitengenezwa kwa
kutumia nyuzi za asili kama vile kamba za mimea na magamba
ya miti. Pia, zilitumia mitego iliyotengenezwa kwa kutumia mianzi
na fito. Wavuvi wengine walitumia mimea iliyokuwa na dawa ya
kulevya samaki, kisha kuwavua. Vilevile, ndoano zilitumika katika
shughuli za uvuvi. Nyavu na mitego vilitumika kunasa samaki
wakubwa na wadogo. Mitumbwi na ngalawa iliyojengwa kwa miti
ilitumika katika shughuli za uvuvi. Vyombo hivi vilitumika kwa
ajili ya kusafiria kwenye maji yenye kina kirefu ili kuvua samaki
wengi na wakubwa zaidi. Pia, dau za asili zilitumika kwa ajili ya
shughuli za uvuvi na usafiri katika bahari na mito mikubwa.
Ugunduzi wa chumvi na moto pia ulisaidia zaidi katika maendeleo
ya shughuli za uvuvi. Chumvi na moto vilitumika kuhifadhia
samaki kwa matumizi ya baadaye. Kwa ujumla, matumizi ya
vifaa na zana katika shughuli za uvuvi na ugunduzi wa chumvi
na moto vilisaidia maendeleo katika shughuli za uvuvi. Jamii za
wavuvi zilivua samaki wengi na kuwa na ziada.
Wavuvi walibadilishana ziada ya samaki na wakulima ili kupata
nafaka. Pia, walibadilishana samaki ili kupata nyavu za kuvulia
84
06/11/2024 11:30:12
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 84
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 84 06/11/2024 11:30:12