Page 82 - Historiayatznamaadili
P. 82
Maadili katika sayansi na teknolojia asilia kabla ya ukoloni
Jamii za kale zilizingatia maadili katika sayansi na teknolojia
za asili. Miiko, kanuni na taratibu ziliwekwa na jamii katika
utayarishaji, matumizi na mwendelezo wa sayansi na teknolojia
FOR ONLINE READING ONLY
asilia ndani ya jamii. Maadili haya yaliheshimu mifumo ya maarifa
na ujuzi asilia, ibada na utamaduni wa jamii. Maadili yalizingatia:
(a) Kurithishwa maarifa na stadi kwa vizazi na vizazi. Hii
ilisaidia mwendelezo wa sayansi na teknolojia ya asili kwa
vizazi vijavyo;
(b) Mgawanyo wa maarifa na ujuzi katika jamii. Hii ilizingatia
zaidi mazingira na uwepo wa rasilimali maalumu katika
jamii. Mfano, wapo waliojifunza uhunzi, uvuvi, uchongaji,
ususi, tiba asilia na kadhalika;
(c) Heshima. Jamii ziliheshimu maarifa na stadi katika sayansi
na teknolojia za asili. Jamii zilitambua uwapo wa wataalamu
na mafundi katika nyanja mbalimbali za sayansi na teknolojia
asilia;
(d) Ushirikiano na uhusiano katika utendaji wa kazi.
Ushirikiano na uhusiano ulifanyika ili jamii kunufaika na
sayansi na teknolojia toka jamii zingine;
(e) Utunzaji wa mazingira. Sayansi na teknolojia asilia
zilitumia njia ambazo zilipunguza athari katika mazingira,
kukuza uhifadhi wa wanyama na mimea, na kuheshimu
uumbaji katika mazingira waliyoishi. Kwa mfano, kwa jamii
za wawindaji ilikuwa mwiko kuwinda mnyama ambaye si
kwa ajili ya chakula au matumizi ya ngozi yake. Pia, ilikuwa
ni mwiko kwa jamii kukata miti ya matunda au ambayo
ingetumiwa na wachongaji. Jamii zilikuwa na maarifa ya
kutambua miti, mimea na matumizi yake. Miiko iliyozuia
kukata miti eneo fulani ililenga kuwezesha uwapo wa
rasilimali endelevu;
(f) Afya ya jamii. Sayansi na teknolojia za asili zilizingatia
afya za wengine. Kwa mfano, wachongaji walihakikisha
miti waliyotumia kuchongea vyombo vya nyumbani ni
75
06/11/2024 11:30:10
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 75
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 75 06/11/2024 11:30:10