Page 78 - Historiayatznamaadili
P. 78
Sayansi na teknolojia za uhifadhi vitu zilifanyika kwa kutumia
chumvi, moto, moshi, jua au mafuta. Uhifadhi kwa kutumia
chumvi ulifanyika kwa kupaka au kunyunyiza chumvi kwenye
nyama na samaki ili kuzihifadhi sizioze. Pia, chumvi ilitumika
kuhifadhi maiti, ambapo chumvi ilipakwa na kunyunyizwa
FOR ONLINE READING ONLY
sehemu mbalimbali za maiti ili kuizuia isiharibike. Sayansi na
teknolojia ya uhifadhi vitu kwa kutumia jua, ilifanywa kwa kuanika
vitu juani ili kuvikausha visiharibike. Vitu kama nyama, samaki au
mboga za majani vilianikwa juani kwa muda mpaka vilipokauka.
Pia, sayansi na teknolojia ya uhifadhi vitu ilitumia moshi. Moshi
ulitumika kuhifadhi vitu kama vile nyama, samaki na nafaka,
ambapo vitu vilibanikwa juu ya kichanja ili vipate moshi. Vilevile,
moto ulitumika kuhifadhi vitu kama nyama na samaki, kwa lengo
la kubanika, kuchoma kuchemsha na kukausha ili visioze. Mafuta
mbalimbali ya asili kama vile mafuta ya minyonyo yalitumika
kupaka ili kuhifadhia vitu visiharibike.
Zoezi namba 4
Oanisha maneno ya sehemu A na maelezo yaliyopo sehemu
B kwa kuandika jibu sahihi zaidi sehemu ya jibu.
Sehemu A Jibu Sehemu B
(i) Jua (a) kubanika, kuchoma
(ii) Mafuta ya kuchemsha na kukausha
minyonyo (b) kupaka na kunyunyizia
(iii) Moto (c) kupaka
(iv) Chumvi (d) kukausha
(v) Moshi (e) kuanika na kukausha
Sayansi na teknolojia asilia za uhifadhi hazikuwa na madhara
kwa binadamu. Uhifadhi haukutumia dawa zenye kemikali kama
ilivyo sasa, ambapo baadhi zina madhara kwa binadamu.
71
06/11/2024 11:30:05
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 71 06/11/2024 11:30:05
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 71