Page 77 - Historiayatznamaadili
P. 77
Pia, chumvi ilipatikana kwa kukausha maji yenye asili ya chumvi
kwenye jua na mabaki yalizolewa kama chumvi. Jamii zilizotumia
sayansi na teknolojia hii ya kutengeneza chumvi, zilitengeneza
matuta yaliyoitwa mabirika maeneo ya bahari au ziwa yenye maji
FOR ONLINE READING ONLY
ya asili ya chumvi ili kukinga maji. Maji yaliingia kwenye mabirika
hayo wakati wa maji kujaa, kisha maji yalikaushwa kwa njia ya
mvuke wa joto la jua. Mabaki yaliyokauka yalikusanywa kama
chumvi. Kielelezo namba 25, kinaonesha sayansi na teknolojia
ya kutengeneza chumvi kwa kukinga maji kwenye “mabirika” na
kukaushwa kwa jua ili kupata chumvi.
Kielelezo namba 25: Sayansi na teknolojia ya kutayarisha chumvi
Sayansi na teknolojia za asilia katika uhifadhi wa vitu
Jamii za kale zilikuwa na sayansi na teknolojia mbalimbali za
kuhifadhi vyakula na nafaka kwa muda fulani ili visiharibike.
Kazi ya kufanya namba 13
Fanya uchunguzi wa mbinu za asili za uhifadhi wa
vitu kama vyakula, nyama, samaki, mazao na maiti
katika jamii inayokuzunguka.
70
06/11/2024 11:30:05
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 70
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 70 06/11/2024 11:30:05