Page 75 - Historiayatznamaadili
P. 75
mkubwa katika kubaini miti iliyofaa kwa uchongaji na kutengeneza
chombo kilichokusudiwa. Kwa mfano, miti iliyotumika
kutengenezea mitumbwi na ngalawa ilikuwa mikubwa na yenye
sifa ya kutokunyonya maji. Miti iliyotumika kutengenezea vyombo
FOR ONLINE READING ONLY
kama sahani, bakuli, miko na upawa ilitakiwa isiwe michungu
na yenye sumu. Zana zilizotumika kwa uchongaji zilitofautiana
kulingana na chombo kilichokusudiwa kutengenezwa. Mfano,
zana zilizotumika kutengenezea vifaa vya nyumbani, vinyago
na mapambo hazikuwa sawa na zilizotumika kutengenezea
mitumbwi na ngalawa. Kielelezo namba 23, kinaonesha shughuli
za uchongaji.
Kielelezo namba 23: Sayansi na teknolojia ya uchongaji
Baadhi ya jamii zilikuwa na sayansi na teknolojia ya kutengeneza
mashine mbalimbali. Mfano, jamii za Wahaya zilitengeneza
mashine za kusaga na kukoboa nafaka. Mashine zilitengenezwa
kwa kuchonga gogo kubwa na ndani yake viliwekwa vyuma laini
vilivyopishana ili kuwezesha kusaga kitu. Mashine hizi zilitumika
kusaga na kukoboa nafaka.
68
06/11/2024 11:30:03
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 68 06/11/2024 11:30:03
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 68