Page 70 - Historiayatznamaadili
P. 70
Vyombo vilivyofinyangwa vilikaushwa kivulini au kuchomwa
kwa moto mkali wa kuni ili viwe vigumu. Vyombo vya mfinyanzi
vilivyochomwa vilipoozwa kwa maji ya baridi. Baadhi ya
wafinyanzi walivipamba vyungu kwa kuvichora kwa mapambo ya
FOR ONLINE READING ONLY
rangi vikiwa vibichi na wengine walivipamba baada ya kukauka.
Kwa mfano, jamii ya Wafipa na Wakisi walipamba vyungu baada
ya kukauka. Kielelezo namba 15, kinaonesha baadhi ya vyombo
vya mfinyanzi.
Kielelezo namba 15: Vitu vilivyofinyangwa katika maumbo mbalimbali
Kielelezo namba 16, kinaonesha mfano wa chungu
kilichofinyangwa na kukaushwa kivulini.
Kielelezo namba 16: Chungu kikikaushwa kivulini
63
06/11/2024 11:29:59
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 63 06/11/2024 11:29:59
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 63