Page 50 - Historiayatznamaadili
P. 50
Sayansi na teknolojia katika Zama za Mawe
Zama za Mawe ni kipindi cha awali kabisa cha maisha ya
binadamu ambapo binadamu alitumia mawe kutengeneza zana.
Sayansi na teknolojia asilia ya utengenezaji wa zana za mawe
FOR ONLINE READING ONLY
ilifanyika kwa kuponda, kupiga, kusugua au kuchonga mawe ili
kupata zana kwa matumizi ya jamii. Zana za mawe zilitumika
katika uwindaji wa wanyama na ndege, kuchimba mizizi,
kuangua matunda na kuchuna ngozi za wanyama. Pia, zilitumika
kutengeneza mavazi ya asili yaliyotokana na magome ya miti na
ngozi za wanyama. Sayansi na teknolojia za utengenezaji wa
zana za mawe, zilitofautiana katika vipindi vya Zama za Mawe:
Zama za Mawe za Kale, Zama za Mawe za Kati na Zama za
Mawe za Mwisho.
Zama za Mawe za Kale
Kazi ya kufanya namba 1
Fikiri mazingira ambayo jamii haina zana au kitu
chochote cha kurahisisha utendaji wa kazi. Je,
maisha yangekuwaje?
Zama za Mawe za Kale ni nyakati za awali za maisha ambapo
binadamu alianza kutumia zana za mawe. Sayansi na teknolojia
ya asili katika utengenezaji wa zana hizo ilifanyika kwa kuchonga
na kuponda mawe ili kupata umbo lenye ncha kali. Kielelezo
namba 1, kinaonesha sayansi na teknolojia ya asili katika
kutengeneza zana za mawe katika Zama za Mawe za Kale.
43
06/11/2024 11:29:49
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 43 06/11/2024 11:29:49
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 43